Burudani

Kanye asimamisha taxi kupiga picha na paparazzi aliyevaa t-shirt iliyomvutia, t-shirt zanunuliwa kama njugu

Kanye West hana urafiki na paparazzi.. lakini paparazzi mmoja amemvutia rapper huyo.

1030-sub-kanye-west-splash-5
Kanye West akiwa na paparazzi ambaye rapper huyo aliyependa t-shirt yake

Akiwa kwenye mitaa ya jiji la New York, Alhamis wiki hii ndani ya taxi, Yeezy aliamua kusimama na kushuka kumpiga picha paparazzi aliyekuwa akimpiga picha kwakuwa alipenda tu t-shirt aliyokuwa amevaa.

rs_560x415-141030095645-1024-kanye-west-dnine.ls.103014_copy (1)
Kanye: T-shirt kali sana hiyo dogo, umenunua wapi?

Kanye pia alipiga picha kadhaa na paparazzi huyo sharobaro. Matokeo ya tukio hilo ni kwamba kampuni inayotengeneza t-shirt hizo imeneemeka baada ya mauzo kuongezeka ghafla.

Kampuni hiyo iitwayo D9 Reserve iliuza zaidi ya t-shirt 300 ambapo kila moja ni dola $135 ndani ya saa chache tangu Kanye afanye uchawi wake!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents