Habari

Kanisa lachomwa moto visiwani Zanzibar, ni siku chache tu baada ya Padre kuuawa

Kanisa

Ikiwa ni siku chache tu baada ya watu wasiojulikana kumuua kwa risasi Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki visiwani Zanzibar, leo alfajiri kanisa moja la kilokole limechomwa moto.

Kwa mujibu wa Kamishna wa polisi mjini MUSA ALI MUSA, baadhi ya viti vya kanisa vimeungua na kwamba moto huo uliwahiwa kuzimwa kabla ya kusababisha madhara zaidi.

Moto huo ulitokana na kurushwa kitu kama bomu kilicholipuka lakini majirani waliamka na kuuzima moto huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents