Habari

Kampuni ya ndege ya Korea kusitisha safari zake za Kenya kwa hofu ya Ebola

Kampuni ya ndege ya Korea imesema itasitisha safari za ndege zake kwenda nchini Kenya kuanzia Agosti 20 Kufuatia hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

korean air

Korean Air Lines Co Ltd imesema kuwa ndege zake zimekuwa zikifanya safari mara tatu kwa wiki kutoka Incheon, Korea Kusini kwenda Nairobi.

Hatua hiyo imekuja baada ya shirika la afya duniani kutahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.

Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.

Source: Reuters/BBC Swahili

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents