Habari

Kampuni ya LG yazindua smartphone mpya yenye screen 2

Kampuni inayotengeneza vifaa vinavyotumia umeme ya LG, imezindua simu zake mpya aina ya LG G6 yenye kioo kimoja kikubwa ambacho kina uwezo wa kutumiwa mara mbili kwa wakati mmoja.

Simu hizo zimeongezewa uwezo mkubwa ambapo zinatumia mfumo wa 18:9 tofauti na simu za kawaida zinazotumia mfumo wa 16:9. Kioo cha LG G6 kina upana wa sentimita 14.5 tofauti na LG5 ambayo ilizinduliwa mjini Barcelona iliyokuwa na upana wa sentimita 13.5 ambapo kampuni hiyo imekiri kuwa simu hiyo haikufanya vizuri sokoni.

Msemaji wa kampuni hiyo Frank Lee amesema, “We started by placing these two [sources] as far apart as possible and then built the phone around it.”

Simu ya LG G6 imepewa uwezo mkubwa zaidi ambapo ina uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa takribani nusu saa bila ya kupata tatizo lolote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents