Habari

Kambi ya Clinton kushinikiza kuhesabiwa upya kwa kura za majimbo matatu Marekani

Kampeni ya Hillary Clinton, Jumamosi hii imedai kuwa itaungana na jitihada za kutaka kuhesabiwa kwa kura katika baadhi ya nchini Marekani, zilizoanzishwa na mgombea wa Green Party, Jill Stein, aliyekusanya mamilioni ya dola ili kura katika jimbo la Wisconsin zihesabiwe upya.

Hillary Clinton and Donald Trump are tightening their grips on the Democratic and Republican presidential nominations.
Hillary Clinton and Donald Trump are tightening their grips on the Democratic and Republican presidential nominations.

Hata hivyo mshauri wa kampeni hiyo, Marc Elias, amedai kuwa uchunguzi wao wenyewe haujaweza kubaini ushahidi wowote wa udukuzi katika mifumo ya kupiga kura.

Elias amedai kuwa licha ya kampeni yake kutopinga matokeo, imeamua kushiriki katika jitihada za kuhakikisha kuwa matokeo hayo yako sawa kwa pande zote. Hata hivyo Rais mteule, Donald amepinga kurudiwa kwa uhesabuji kura na kusema kuwa uchaguzi umemalizika.

“The people have spoken and the election is over, and as Hillary Clinton herself said on election night, in addition to her conceding by congratulating me, ‘We must accept this result and then look to the future,'” alisema Trump kwenye maelezo yake.

Trump pia amekikosoa Green Party na kudai kuwa jitihada zake ni za ulaghai huku akimshutumu mgombea wake, Jill Stein kwa kutaka kujikusanyia fedha ambazo hatozitumia kwa shughuli hiyo.

“This recount is just a way for Jill Stein, who received less than one percent of the vote overall and wasn’t even on the ballot in many states, to fill her coffers with money, most of which she will never even spend on this ridiculous recount,” amesema Trump.

“This is a scam by the Green Party for an election that has already been conceded, and the results of this election should be respected instead of being challenged and abused, which is exactly what Jill Stein is doing.”

Stein amekanusha shutuma za Trump kuwa hatozitumia fedha hizo kwa kuhesabiwa upya kwa kura. “For his information, this is all going into a dedicated and segregated account so that it can only be spent on the recount,” aliiambia CNN.

Kampeni ya Clinton imekutana na wanasheria, wataalam wa data na wachambuzi kukagua kama kulikuwepo na udukuzi katika matokeo.

Hadi sasa Clinton anaongoza kwa kura milioni 2 za kawaida dhidi ya Trump.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents