Burudani

Kama kweli wewe ni kioo cha jamii, tunajifunza nini kutoka kwako?

Ukweli unauma sana hasa unapo kuhusu wewe binafsi, unatamani ukweli huo aambiwe mtu mwingine bali linakuhusu wewe kama msanii, kiongozi wa serikali, dini , shirika n.k. Hapa Bongo tumezoea kusikia ‘Mimi ni kioo cha jamii’ au wasanii ni kioo cha jamii kwa kuwa wanajaribu kuonyesha mambo yanayoendelea kwenye jamii katika sanaa zao za nyimbo , mashairi na maigizo na vitu vingine ambavyo inawezekana sivifahamu.

elle-07-cover-break-rihanna-v-xln

Nimekuwa nikijiuliza na kujitizama kwenye kioo hicho hicho ambacho kinaitwa cha jamii nimeshindwa kuelewa au ninatizama vibaya na mara nyingine natamani kujificha chini ya uvungu kwani kioo kinachoitwa kioo cha jamii si kioo cha jamii bali ni balaa la jamii.

Je mambo yanayoendelea kwenye wasanii wetu na viongozi wetu je ni kioo cha jamii? Ukifuatilia vyombo vya habari vingi utakutana na habari nyingi kuhusu wasaniii wetu. Habari zao nyingi si nzuri wala hazipaswi hata  kuongelewa, kwani wanachokifanya ni tofauti sana au hakielekeani kabisa na ujumbe ambao wamekuwa wakituletea sisi tunaowatizama au kufuatilia kazi zao. Kama maisha yao tu binafsi hayawezi kuelimisha jamii itakuwaje wimbo wako ubadilishe jamii? Au ni sawa sawa na kuimba kwamba madawa ya kulevya si mazuri katika jamii yetu wakati wewe ndio msafirishaji na muuzaji huku mtumiaji mwenyewe?

Hakuna sehemu yeyote duniani ambayo unaweza kusema kwamba wewe ni mwizi au mla rushwa halafu ukaendesha kampeni ya kuzuia rushwa ikafanikiwa. Hiyo itakuwa ndoto siku zote, hivyo kabla sisi wenyewe ambao tunajiita kioo cha jamii hatujaelimisha watu wengine tunatakiwa tuonekane tumeelimika katika hicho tunachotaka kuelimisha. Mfano mzuri ni kwamba haina mantiki wewe ukiimba wimbo wa mapenzi ya dhati huku una kashfa kibao za za ufuska na mazingira ya kutoonyesha mapenzi ya dhati.

Je Mnataka tuamini kwamba mnaishi maisha ya Uongo? Huu ni mtizamo tu kwamba kama sanaa unayofanya haiendani na maisha halisi ni kwa ajili ya faida ya nani? Huoni kwamba unapata shida ya kufanya kitu ambacho hata hujawahi kujua inakuwaje kuwa katika hali hiyo wakati wewe mwenyewe yamekushinda? Kama kweli sisi ni kioo cha jamii inatupasa kuchukua hatua ya msingi na kufanya maamuzi ya kuhakikisha ujumbe tunaoipelekea jamii unaendana na maisha yetu halisi hapo ndipo watu watatuaona kama kioo cha jamii. Kwa sasa wengine wanaonekana ni balaa la jamii, hivyo tunatakiwa kuitendea haki jamii ambayo tunasema sisi ni kioo cha jamii hiyo.

Kitu kingine cha msingi, Je wasanii wetu wanalelewa na nani? Nani ni mshauri wao kitaaluma na kimaisha? Hatua za msingi sizipofanyika tutaendelea kupoteza wasanii wengi kutokana na kwamba hakuna mshauri wa maisha yao binafsi. Hivyo wanaishi vile wanafikiri ni sahihi bila kujua maisha na taaluma zao zinaathirikaje na maamuzi yao ya kila siku. Wasanii wengine mnaweza kujifunza tu kwa waimbaji wa nyimbo za injili utagundua wale ambao wako chini ya washauri wazuri wanaendelea vizuri sana na wale ambao hawana washauri wamekuwa wakifanya vitu vya ajabu. Ili ufike mbali unahitaji watu wa kukushauri vizuri na unahitaji kunyenyekea, kiburi hupoteza watu wengi na kuharibu taaluma yako na mwisho unafikia kufanya maamuzi ambayo hupati msaada kwa watu wengine. Je wewe ni kioo cha jamii?

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents