Burudani

Kalapina adai akiwa mbunge hatosita kutoa kichapo kwa wenzie watakaomletea upuuzi

Rapper Kalapina ambaye anatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuusaka ubunge wa jimbo la Kinondoni, amesema kuwa akipata fursa hiyo hatosita kusambaza kichapo kwa wabunge wenzie pindi wanapokuwa na malumbano ndani ya mjengo.

KalaPina-620x350

Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Kalapina amedai kuwa atatembeza ‘nakozi’ kwakuwa anatambua hakuna sheria inayoweza kumbana kutokana na kufanya tukio kama hilo.

“Vitasa kidogo, wewe ile hela imepigwa Tegeta huko na Tegeta hakuna mtu kachukua hata shilingi, vitasa vingetembea,” alisema. “Nafikiri ulimuona mheshimiwa Sugu, si unatetea watu na mbunge ndani ya bunge huwezi sijui kupelekwa mahakamani, masula yanamalizwa kibunge,” aliongeza.

“Kwahiyo ngumi bungeni zipo, mabunge yote duniani, sema bunge letu halijapata wale watu ambao wanaweza kupigana vita na mtu mwenyewe ni Kalapina mgombea wa Kinondoni ninayeingia mjengoni, Jamanii eeh jipangeni, nakuja huko.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents