Bongo5 MakalaBurudani

Kalamu ya Nick wa Pili: Thamani ya Sanaa ni Kikiii?

Imeandikwa na rapper Nick wa Pili,

Nakutana na wasaniii wachanga wengi, kwenye show, mitandaoni, mtaani, studio na wengine wananipigia simu. Wengi huomba kolabo, ushauri, namba za simu za watu mbalimbali wa kwenye industry hii. 80% huomba ushauri wa kutoka, kolabo kwa dhana ya kuwasaidia kujulikana mapema, ama kusaidiwa kufikisha CD zao kwa watu fulani fulani.

nickiiiiii
Nick wa Pili

Ni Ngumu sana kukutana na msanii mchanga akakuuliza namna ya kuboresha uwezo wake wa kurap, kuimba ama kuwa mwandishi mzurii…kwa kifupi kuwa msanii bora.

Msanii wa kwenda kwenye concert anataka kwenda studio, msanii ana nyimbo moja na nusu anataka umtafutie dili ya kurekodi. Mimi mpaka naenda studio nilikuwa nimeshaperfom matamasha mengi ya kushindanisha vipaji na nilikuwa na nyimbo mbili mpya kila wiki. Hazikuwa kali ila ndio zilikuwa hatua za kujifunza kurap na kuandika mashairi.

Wakati natafakari nini msingi wa sanaa kuonekana rahisi namna hii na kuwa maarufu kuwa ndio inspiration kwa wasaniii wachanga na wala sio usaniii bora, nikawasha TV mara nikaona nyimbo ya kiwango sawa kabisa na jamaa mmoja ananiimbiaga nikienda saloon. Ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo.

Theni ikaja interview, mtangazaji anamuuliza msanii ‘kwa nini muziki haulipi?’ Nikacheka, utalipaje wakati ni kitu rahisi sana na hata nikitoka nje tu hapo hata mfanyakazi wako wa ndani anaimba sawa tu na unayemuona kwenye TV? Hamna kitu kisicho na thamani kinacholipa….kitu ambacho sina uhakika ni kama na yeye akiwa ghetto kwake huwa anaangalia playlist anayoipanga.

Ni biashara binafsi sio sahihi kumjaji mtu kwa anachofanya, lakini je haujisikii furaha kipindi ulikuta una mashabiki 200 ukafanya wakawa 2,000, loyal fans? Hautajisikia furaha kizazi kinachofuata nao wakaja kalia kiti hicho? Biashara zetu ni binafsi lakini jamii yetu sio na ni jukumu letu la ujumla kuandaa mazingira bora kwa watoto na wadogo zetu.

Anyway turudi kwenye mada. Natafakari watu kama Kendrik Lamar, 50 Cent, iliwachukuwa si chini ya miaka 10 kufika mainstream. Kina Keri Hilson miaka 5 ya kuwa backup singer. Ninakakumbuka mfuko wa Joh Makini uliokuwa umejaa mashairi tumeutundika pale sebuleni kwetu.

Nikakumbuka kuwa gemu ya muziki wa kizazi kipya ina kama miaka 15 ila ina zaidi ya wasanii 50 waliowika na kupotea wakati Nas, Snoop, Jay Z, wanakaribia miaka 20 kwenye game on top. Radio kama Hot 97 na host kama Funk Master Flex, toka miaka ya 90 mpaka leo wanakimbiza New York, source magazine. Halafu nawaza baadhi ya vipindi vikubwa vilivyopoteza umaarufu hapa bongo, shows za TV ambazo nilikuwaga naziota kuwepo.

Sikumbuki mara ya mwisho nimeaangalia lini shows za kujaza Diamond Jubilee. Msanii mmoja ndio alikuwa na thamani ya show moja ya club, leo ni wasanii 8.

Thamani au value…hujengwa na nini na hujengwa na nani? Unawezaje kuilinda kulingana na mabadiliko ya muda na tamaduni za kinyakati?

Toa maoni yako ukiyaelekeza kujibu maswali hayo.

Unaweza kuni mention kupitia akaunti yangu ya Twitter, Nick Mweusi: @nikkwapili, ama Instagra, @nikkwapili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents