Burudani

Kala: Mwaka huu nimeingiza kipato kikubwa kuliko miaka yote. Akanusha kupotea kwenye game

Hit maker wa ‘Dear God’, Kala Jeremiah amepinga vikali kuwa amepotea kwenye game toka alivyohit na wimbo wa ‘Dear God’, huku akidai kuwa huu ndio mwaka ambao ameingiza pesa nyingi kuliko miaka mingine aliyokaa kwenye muziki.

Kala Jeremiah Walewale_full

Akizungumza na Bongo5 leo, Kala amesema licha ya kutoonekana akifanya show kwa wingi mwaka huu, lakini ameingia mikataba mingi na makampuni mbalimbali.

“Mwaka huu ni mwaka mzuri kwangu kuna mikataba nimeingia, si kweli sijapotea, ni mitazamo ya watu, ukweli ni kwamba mwaka huu kwangu umekuwa mwaka wa baraka, wa neema mwaka wa mavuno kwahiyo ni mwaka mzuri kwangu ninaweza kusema. Kibiashara nimefanya vizuri mwaka huu, inawezaka mwaka huu nikawa sijafanya show nyingi lakini kifedha nadhani au kwa kipato mwaka huu ninaweza kusema nimeingiza kipato kikubwa kuliko miaka yote niliyokuwa kwenye muziki,” alisema Kala.

Katika hatua nyingine Kala amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiri muziki mzuri kabla mwaka huu haujaisha.

“Mashabiki wasubiri muziki mzuri tu, siwezi kusema ni ngoma gani inakuja wao wasubiri wataona,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents