Awards

Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz, Diamond na Chalz Baba waibuka na tuzo nyingi zaidi kwenye KTMA 2013

Rapper wa Mwanza, Kala Jeremiah amefanikiwa kuibuka na tuzo tatu ikiwemo kubwa ya wimbo bora wa mwaka kwa hit yake ‘Dear God’. Kala alishinda pia tuzo ya msanii bora wa Hip Hop kwa kuwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Stamina kwenye kipengele hicho.

IMG_4289

Naye Ommy Dimpoz ameibuka na tuzo tatu zikiwemo za wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa kwa hit single yake Me and You. Pia hit yake Baadaye imechukua tuzo ya video bora ya mwaka.

IMG_4325

Licha ya kutokuwepo wala kutuma mwakilishi, Diamond alifanikiwa kushinda tuzo kubwa ya pili kwa usiku huo ya msanii bora wa kiume kwa kuwabwaga Ben Pol, Linex, Mzee Yusuf na Ommy Dimpoz na pia kushinda tuzo ya Msanii bora wa kiume Bongo Flava.

Tuzo za muziki wa dance zilitawaliwa na Chalz Baba wa Mashujaa Band aliyeibuka tuzo mbili za Msanii bora wa kiume Bendi na Mtunzi bora wa mashairi – Bendi.

Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.

Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.

Hii ni list nzima ya tuzo hizo.

Wimbo bora wa mwaka

Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume

Diamond

Msanii bora wa kike
Lady Jaydee

Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi

Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf

Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava

Recho

Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah

Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba

Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu

Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe

Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz

Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf

Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop

Kala Jeremiah

Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba

Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter

Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico

Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso

Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta

Rapper bora wa bendi
Fagasoni

Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto

Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band

Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego

Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha

Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab

Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa

Wimbo bora wa zouk rhumba
Ni wewe – Amini

Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab

Jahazi Modern Taarab

Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad

Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje

Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents