Burudani

Kala Jeremiah kuhusu BSS: Ni ngumu kupata vipaji kwa kuimba copy

Rapper Kala Jeremiah ambaye wimbo wake mpya Dear God unafanya vizuri kwenye radio na TV, amesema washindi wa Bongo Star Search hushindwa kufanya vizuri baada ya shindano hilo kwakuwa mfumo wa washiriki kuimba copy za wasanii wengine hautoi vipaji vya kweli.

Amesema kuimba nyimbo za watu ni kitu rahisi ambacho kila mtu anaweza kukifanya.

“Washiriki pale wanafanya nyimbo za watu, wakitoka pale wanatakiwa wakafanye nyimbo zao sasa unajua kucopy nasikiaga hata watu wanaoosha vyombo wanaimba vizuri sana nyimbo za watu lakini haimaanishi kuwa ni msanii kuimba wimbo wa mtu vizuri.Kuna mtu mwingine ana kipaji hicho kwamba anaweza kukifanya kitu perfect na sio mzuri kihivyo,” amesema Kala.

Amesema ifikie wakati BSS ianzishe utaratibu wa kuwapeleka studio wasanii kumi bora ili waimbe nyimbo zao ama kuwapigia live nyimbo walizotunga wenyewe ili kujua wasanii wenye uwezo wao wenyewe.

Hata hivyo amesema BSS ya sasa hivi imeandaliwa vizuri tofauti na enzi zao.

“Sisi kiukweli tulifanya kimaskini nadhani hilo liko wazi sababu ilikuwa mwanzo na siku zote mwanzo ni mgumu. Sasa hivi wameadvance sana yaani wamefikia hatua ambayo natamani sasa mimi ndio ningekuwa BSS sasa hivi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents