Burudani

Kala Jeremiah anusurika kifo, apata ajali usiku wa jana akitokea kwenye show ya Valentine

Siku ya jana ambayo ilikuwa ni February 14 siku ya wapendanao msanii wa ‘Dear God’ Kala Jeremiah, aliimaliza kwa mkosi baada ya kupata ajali ya gari akiwa njiani akitokea kwenye show ya Valentine iliyofanyika Club East 24.

kala2

Kupitia Instagram rapper huyo ambaye kwa sasa ana single inayoitwa ‘Wale wale’ , alipost picha ya gari yake ikiwa imeharibika ubavuni baada ya ajali hiyo na kuandika ujumbe huu:

kala ajali

‘nIMEPATA AJALI USIKU HUU NIKIWA NATOKEA CLUB EAST 24 AMBAKO NILIKUWA NAFANYA SHOW NA B BAND WAKATI NARUDI NYUMBANI NIKIWA NIMEKARIBIA KABISA NYUMBANI GHAFLA KUNA MTU WA PIKI PIKI AKAWA ANATAKA KUINGIA NIKAJARIBU KUMKWEPA GARI ILIKUWA KWENYE MWENDO KASI KIDOGO IKAYUMBA KWENDA KULIA NIKAIRUDISHA IKARUDI ZAIDI KUSHOTO NIKAIRUDISHA TENA KULIA IKAWA INATAKA KWENDA MTARONI NIKAIRUDISHA TENA KUSHOTO AMBAKO ILIGEUKA ILIKUKUA INATOKA NA KUINGIA MTARONI AMBAKO ILIKITA NA KUVUNJA MLANGO WA UPANDE WANGU.SIJAAMINI KAMA NIMETOKA BILA HATA JEREHA MGUUNI WALA MAUMIVU ZAIDI YA YALE UA KICHWANI KIDOGO NILIYOJIGONGA KWENYE MLANGO KWA JUU. ASANTE SANA MUNGU UMENIOKOA. ASANTE SANA MUNGU WANGU’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents