Burudani

Kala Jeremiah: Album mpya mpaka miaka mitano ijayo

Rapper Kala Jeremiah amedai kuwa kutokana na mauzo mabaya ya album ya Pasaka aliyoitoa mwaka jana, hafikirii kutoa tena nyingine hadi miaka mitano ijayo.

Kala Jeremiah Walewale_full

Kala amesema sababu kubwa ya kufanya vibaya kwa album yake ni mfumo wanaoutumia wasanii kuuza kazi zao wenyewe.

“Album unajua ni kitu ambacho kinatakiwa kuja automatic,halafu ukiangalia kwa soko la sasa hivi album siyo biashara unaweza sema unaitolea macho upate pesa,unatakiwa ufanye kama automatic,sio kwaajili ya mapato,” Kala ameiambia Bongo5. “Kwa mimi kama mimi,kwa hizi sababu zote naweza kufiria kutoa albam mpaka baada ya miaka mitano. Pia Pasaka bado inafanya vizuri.”

Kala ambaye hivi karibuni aliachia remix ya wimbo wake ‘Wale Wale’ amesema tayari ana nyimbo nne zitakazotoka baadaye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents