Burudani

Kala Jeremiah adai serikali iliyopita haijawanufaisha wasanii

Rapper Kala Jeremiah amesema serikali inayomaliza muda wake haijawasaidia wasanii.

Kala Jeremah

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio rapper huyo amesema yeye kwa upande wake haoni kilichofanywa na serikali huku akisema bado kazi zao zinauzwa mitaani.

“Watu wanatengeza CD ya Kala Jeremiah, anachanganya na msanii mwingine halafu anauza mtaani. Tunakutana nao hao wanakugongea kioo wanakuuzia CD ukiangalia wimbo wako upo kwenye hiyo CD, unafanya nini sasa? Unamkamata mwisho wa siku unaenda unapoteza muda wako kwa sababu hakuna sheria,” alisema.

“Serikali inatakiwa itutambue kwenye hilo na iweke mkazo. Kwa sababu hawa wezi wapo na wanaonekana kwa macho. Kwahiyo serikali ijayo inatakiwa kuleta mabadiliko makubwa hasa hasa kwa nyanja yetu hii ya vipaji. Serikali ijayo mimi nitaidai sana masuala ya vipaji, kwa sababu mimi mwenyewe ni mmoja kati ya waathirika ambao tupo kwenye hili suala,” aliongeza.

“Tunapata mikataba kweli lakini inakuwa imeshachakachuliwa na watu wa kati ambao wako wengi na hauwezi kukwepa kwa sababu huwezi kuipata deal ambayo itakuwa moja kwa moja kwa sababu hizo kampuni zinazotoa deal wana-deal nazo na hao watu wa kati wana interest zao. Kwahiyo naiomba sana serikali iliangalie sana hili kwa manufaa ya wasanii pamoja na serikali.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents