Burudani

Kajala amkingia kifua mwanae, ‘hamjui nimepata tabu gani na mwanangu’

Kajala ni mama mwema kwa mwanae wa kike Paulette aliyeza na P-Funk Majani? Hilo ndio swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza kiasi cha kuwepo wale ambao wamekuwa wakimkosoa hadharani na kusema kuwa anampoteza binti yake.

97a75214abb511e3a3561248e7b87ef4_8
Kajala na mwanae

Kwa mara nyingine tena, muigizaji huyo wa filamu ameamua kujibu tuhuma na matusi anayoyapata kutoka kwa wale wanaohisi haoneshi mfano bora kwa mwanae. Kilichomuudhi zaidi ni kuwa wapo watu wanaomtukana mwanae.

“Nadhani kila binadamu anaufanya kitu anacho penda lkn kama nyinyi wote mnaona mm ninacho fanya nakosea siwezi kuwalaumu, nawaomba mnitukane usiku kucha mkilala nitukaneni mkiamka nitukaneni nimeshazoea nilikuwa naumia mwanzo lkn sasa siumii tena ninacho waomba amjui nimepata tabu gani na mwanangu kwahiyo kama anae wakosea ni mm na sio mtoto wangu basi naomba mnitukane mm na umal*ya wangu msimuingize mwanangu please please nawaomba sana kiroho safi,”
ameandika Kajala.

“I feel the same way as well. lakini don’t expose so much your daughter to social media, I mean don’t post so much pics of her coz that will also affect her,” ameandika mmoja wa followers wake huku mwingine akiongeza ‘The good thing ninakushauri usimruhusu mwanao awe na mazoea na hii mitandao ya kijamii awe busy na masomo yake frm there hatojua nini kinaongelewa juu yake na juu yako.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents