Burudani

Kajala akanusha kumshtaki mama yake Wema

Kajala Masanja amekanusha uvumi ulioandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa amefungua kesi dhidi ya mama yake mzazi na Wema Sepetu kutokana kile kilichodaiwa kutukanwa na mama huyo kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wema mwishoni mwa mwezi uliopita.

FRONTAMANI

Kajala ambaye amesema yupo busy na kazi zake binafsi, ameiambia Bongo5 hana ugomvi wowote na Wema kama watu wanavyozusha. “Hapana sijamfungulia mashtaka yoyote Mama Wema. Siwezi kufanya kitu kama hicho mama ni mzazi, mzazi kama mzazi huwezi ukasema umrudishie kitu,” amesema. “Mzazi anaweza akakutukana akakufanyia nini lakini still atabakia kuwa mzazi. Sina ugomvi wowote na Wema, hayo mambo sasa hivi hayapo ni kazi tu.”

1389132_803381699682221_904009838_n
Wema na mama yake

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents