Habari

Kaimu Jaji Mkuu aahidi kusajili kesi katika mfumo wa kielektroniki

Kaimu Jaji Mkuu, Pro Ibrahim Hamis Juma ameeleza mikakati yake ya kufanya mabadiliko katika mahakama ikiwemo kesi kusajiliwa katika mfumo wa kielektroniki ili kuwezesha haki.

Jaji huyo ameyaeleza hayo Jumatano hii baada ya kuapishwa na Rais wa Jammhuri ya Muuungano wa Tanzania kuwa Kaimu Jaji mkuu wa Tanzania. “Mimi lengo ni kuhakikisha kesi zinasajiliwa zinakuwa katika mtindo wa kielektroniki ili kuwezesha haki iweze kupatikana kwa haraka na kuwa na uwazi zaidi ya ilivyo sasa,” alisema Jaji Juma.

Kwa upande wake Jaji Mstaafu,Mohamed Chande Othuman aliwataka watumishi wa mahakama kufanya kazi kwa uwazi, weledi na kuwashirikisha wananchi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara. Kaimu Jaji Ibrahim Juma amechukua nafasi ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othuman Chande.

BY:Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents