Habari

Dkt Kafumu na Mh Vicky Kamata wajiuzulu

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu katika nafasi zao.

Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.

Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye ofisi ya spika wa bunge jana. Kafumu ni Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) ambapo Vicky Kamata ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akiwakilisha wanawake wa Mkoa wa Geita.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents