Burudani

Kabwela Foundation ya Stamina kuanzisha kipindi cha TV

Msanii wa muziki wa Hip Hop na mmiliki wa Kabwela Foundation taasisi inayojishughulika na masuala ya kutoa misaada kwa wenye mahitaji maalum katika jamii, Stamina, anatarajia kuanzisha kipindi cha TV ili kurusha mambo mbalimbali yanayofanywa na tasisi hiyo.

737291_561095583919966_810953846_o
Akizungumza na Bongo5, Stamina amesema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa kubwa na inahitaji kipindi cha TT ili kuonesha mambo yanayofanywa na tasisi hiyo.

“Tunamshuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, taasisi imepata wadhamini ambao watakuwa wanatoasupport , tunasubiri sikukuu tu tuweze kuintroduce mambo mapya,” amesema Stamina. “Kabwela tayari imeshakuwa kampuni sasa hivi imesajiriwa, tunatarajia kuanzisha kipindi cha TV, na sasa hivi tayari tumeshoot vipindi kama vitano, kwahiyo mambo mengi mazuri yapo njiani. Hivi vipindi vitakuwa vinahusu Kabwela Foundation vitu ambavyo tunavifanya ndani ya foundation vitakuwa vinaonyeshwa kwa hicho kipindi. Kuna TV station moja tumeiomba imetupa ,kwahiyo kila kitu kipo fresh,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents