Burudani

Jux awajibu waliohoji kwanini hajawahi kupost picha yoyote akiwa chuo anakosoma nchini China

Mastaa wengi wamekuwa wakiutumia mtandao wa Instagram kupost picha ambazo zinaonesha maisha yao na karibia kila wanachofanya, lakini kwa msanii wa R&B Juma Jux kuna mstari ambao ameuweka kati ya vitu anavyoshare kwenye mtandao huo na maisha yake binafsi.

jux2

Inafahamika kuwa Jux anasoma nchini China, lakini hajawahi kupost picha yoyote ikionesha yuko kwenye mazingira ya chuo kama ambavyo labda hupost akiwa kwenye bata au akiwa na washkaji zake au kwenye show.

Baada ya kuulizwa kama kuna mambo mengine anayoyafanya huko tofauti na chuo, na kama kweli anasoma ni kwanini hajawahi kushare na mashabiki wake picha zozote za mazingira ya chuo, haya yalikuwa majibu yake.

“Nachoamini mimi hapa unajua mimi katika maisha yangu, Instagram ni profile yangu mimi naamua nifanye nini sifanyi kwasababu ya watu, pia najua mimi ni msanii kuna watu wananiangalia kuna vitu flani siwezi kuvuka nikavifanya, “ Jux aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

“Darasani sio sehemu ya kupiga picha umuoneshe mtu, kwanza darasani kwetu hairuhusiwi kupiga picha, haiwezi kuwa mwalimu yupo anafundisha halafu unapiga nioneshe watu, no. Nazingira yangu ya nje ya chuo ndio nafanya vile haya ni maisha yangu ya nje ya chuo, lakini chuo nikienda naenda kusoma siendi kupiga picha, kama mtu haniamini kwamba mimi nasoma nafanya vitu vingine sina power zaidi ya kushawishi watu waniamini zaidi ya msemo wangu kwamba mimi kule nasoma, siwezi kwenda darasani nipige picha niko na madaftari no, lakini mimi nasoma niko kule kwasababu ya masomo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents