Burudani

Jux ataja kiwango alichotozwa na Mabeste kumwandikia wimbo wake mpya ‘Sisikii’, ni zaidi ya 1M na ameilipa

Wasanii wengi wa bongo siku hizi hawawaandikii bure nyimbo wasanii wenzao sababu imegeuka kuwa biashara inayolipa, kitu ambacho kimemkuta Jux pia ambaye single yake mpya ‘Sisikii’ iliyotoka jana ameandikiwa na rapper Mabeste.

10616924_851357238221592_723195210_n

Akizungumza wakati anautambulisha wimbo huo jana kupitia XXL ya Clouds Fm, Jux amesema alipomfata Mabeste na kumwomba amwandikie wimbo alimwambia atafanya hivyo lakini anataka alipwe kwa kazi hiyo.

“Tukaongea na mabeste akasema gharama zake, akasema mi nitaandika lakini siandiki ngoma bure Jux, nikasema aah huu si muziki bwana, muziki unajua uki invest na kama kitu kizuri hujui baadae itakuwa vipi, nikamwambia sawa akaniambia price yake anayofanya ye Mabeste kuandika nyimbo nikamwambia fresh akachora ngoma na kweli kabisa nikaimba ikaisha…studio tulikuwa mimi Bob na Manecky”.

Jux amesema kuwa amemlipa Mabeste shilingi milioni mbili (2,000,000/=) kwaajili ya kuandikiwa wimbo huo.

“2 million, serious Mabeste aliniambia hivyo sababu ana nyimbo nyingi sana, na kuna nyimbo nyingine mimi nilishindwa kuzichukua kutokana na bajeti yangu…nikampa hela akachora baadae tukatoka nikaenda kwenye ATM nikamtolea hela nikammalizia hela yake”.

Aliendelea,

“Mimi sikutegemea kama angeniambia hiyo hela hata mimi mwenyewe nilishangaa , nime bargain hadi kufika hapo ana nyimbo nyingine ambazo mimi nilikuwa nazitaka kabisa nyimbo kali sana Mabeste anafika hadi 4 million, lakini nyimbo yangu akasema kwa hii nyimbo yako kwasababu beat ni yako, melody umetoa hiyo hapo kama hutaki basi, afu mi nikaangalia nikasema sasa kama mtu unaweza ukalipa video hela nyingi…kwahiyo mi nikaona nataka kitu kipya, muziki mpya ambao kila siku sio yule yule Jux nikamwambia sawa Mabeste.”

Baada ya wimbo kukamilika Jux aliridhika kupata kile alichokilipia, “kwa sababu nyimbo nilivyoiskia wakati imeisha nikaona yah this is a song I needkwahiyo sawa Mabeste umefanya kitu”.

Baada ya kulipishwa na Mabeste, Jux pia amemwimbia Mabeste chorus ya wimbo wake mpya ambao naye amemlipisha.

“Kuna chorus yake ambayo inakuja mi nimemfanyia Mabeste..hiyo ni biashara yeye ameni charge na mimi nimemcharge tunafanya kibisahara zaidi”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents