Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Juventus na Monaco mbele kwa mbele UEFA, Barca na Dortmund nje

By  | 

Timu za Juventus na Monaco zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya (Uefa) usiku wa Jumatano huku zikiungana na Real Madrid na Atletico Madrid ambazo zilifuzu katika hatua hiyo siku ya Jumanne.

Juventus imefanikiwa kuingia katika hatua hiyo kwa kuitoa Barcelona ya Hispania kwa jumla ya mabao 3-0 ambayo walishinda katika mchezo wao wa kwanza wiki iliyopita huku katika mchezo wa jana wakitoka sare ya 0-0.

Nao Monaco wametinga hatua hiyo kwa kuitoa Borussia Dortmund kwa jumla ya mabao 6-3 ambapo katika mchezo wa kwanza walishinda magoli 3-2 na katika mchezo wa jana katika uwanja wao wa nyumbani wa Stade Louis II waliibuka tena na ushindi wa mabao 3-1.

Katika mchezo huo magoli ya Monaco yalifungwa na Mbappe dakika ya 3, Falcao dakika ya 17 na Germain dakika ya 81 huku goli la kufutia machozi la Dortmund likifungwa na Reus dakika ya 48.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW