Burudani

Justin Bieber awaudhi Wachina na Wakorea kwa kupost picha ya kanisa la Japan lenye utata, aomba radhi

Justin Bieber amekinukisha tena. Safari hii si kwa kujua na ni baada ya kuwaudhi Wachina na Wakorea Kusini kwa kupost picha kwenye Instagram ya kanisa lenye utata la nchini Japan.

article-2611045-1D48E3E300000578-670_634x818
Picha hiyo inamuonesha Justin Bieber akiwa mbele ya kanisa hilo na kuandika: “Thank you for your blessings.”

Staa huyo wa Canada aliweka picha ya kanisa hilo la Yasukuni la jijini Tokyo ambalo ni kumbukumbu ya watu milioni 2.5 waliouwa miongoni mwao wakiwa wahalifu wa kivita. Kanisa hilo ni tata kwa nchi za China na Korea Kusini ambalo wanaliona kama kitu cha Japan kujivua udhalimu na ukatili ulioufanya pale ilipoyashika maeneo mengi ya China na Korea wakati wa vita vita vya pili vya dunia.

article-2611045-1D49664000000578-920_634x637

Baada ya watu wengi kumshambulia kwenye Instagram, Bieber aliifuta picha hiyo na kuandika post nyingine ya kuomba radhi kwa kuandika: “While in Japan I asked my driver to pull over for which I saw a beautiful shrine. I was mislead to think the shrines were only a place of prayer. To anyone I have offended I am extremely sorry. I love you China and I love you Japan.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents