Tragedy

Mabaki ya ndege ya Air Algerie iliyoanguka yapatikana nchini Mali

Mabaki ya ndege ya Air Algerie iliyokuwa na watu wa 116 na kupotea mapema jana, yamepatikana nchini Mali karibu na mpaka na Burkina Faso.

140106-AirAlgerie737800-01

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na ikulu ya Elysée ya Paris, Ufaransa ndege hiyo imethibitika kuwa ilianguka. Ilisema kuwa vikosi vya majeshi ya Ufaransa vilivyopo nchini Mali vipo njiani kuelekea kwenye eneo ilipoangukia ndege hiyo, katika mkoa wa Gossi, kusini magharibi mwa mji Gao, nchini Mali.

Kulikuwa na raia 51 wa Ufaransa kwenye ndege hiyo ya Boeing MD-83. Rais wa Ufaransa, François Hollande jana alidai kuwa ni ngumu kubaini chanzo cha ajali hiyo.

“Tunachojua ni kuwa marubani walitoa taarifa kuwa walitaka kubadilisha muelekeo kutokana na hali mbaya ya hewa,” alisema. Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita anatarajiwa kwenda kutembelea eneo la ajali leo.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, kwenda mjini Algiers. Hiyo ni ajali ya tatu ya ndege kutokea katia kipindi kifupi mwezi huu baada ya ile ya Malaysia Airlines MH17 iliyodunguliwa na waasi mashariki mwa Ukraine na kuua watu zaidi ya 200 pamoja na ndege ya Taiwan iliyoua watu 48.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents