Michezo
Jurgen Klopp asherehekea kumnasa Sadio Mane
Klabu ya Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Southampton Sadio Mane kwa pauni milioni 30 kwa mkataba wa wa miaka mitano.
Mane amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Liverpool Jumanne baada ya kwenda Merseyside kufanya vipimo vya afya na pia kuketi na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ian Ayre kwaajili ya maslahi yake binafsi na akakabidhiwa jezi namba 19.