Habari

Juma Nature: Wanawake wengi waongo, bado nipo nipo sana

Juma Nature amesema tabia ya uongo kwa wanawake wengi inamfanya asifikirie kuoa awe mgumu kuoa.

Juma Nature

Nature ambaye ni baba wa mtoto mmoja aitwaye Furaha, ameiambia Bongo5 kuwa anashidwa kufanya uchaguzi sahihi wa mwanamke kutokana na wanawake kuwa matapeli.

“Suala la kuoa ni suala la kitaifa, siku mimi nikioa hata rais atajua Juma Nature anaoa, nikiwa tayari hata rais atafahamu kwamba mchizi anachukua jiko.”

“Mimi kuoa bado sana, nashukuru mungu sasa hivi nina mtoto ‘Furaha’ anasoma vizuri anaongea kiingereza mpaka kichina. Tatizo linalonifanya nisioe na ni nisifirie kuoa ni watu hawakai ndani, watu waongo sana sasa hivi, sasa hivi wanawake wengi sana waongo waongo, unaweza ukasema nifanye naye maisha kumbe ndo cheche huyo. Sasa utaoa vipi wakati kila unayekutana naye unamuona kabisa huyu ni tapeli.”

Pia Nature amewaka watanzania kuendelea kusupport wimbo wake mpya unaoitwa Komaa uliotoka sambamba na video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents