Michezo

Juma Kaseja kuikosa mechi dhidi ya Simba SC

Kocha mkuu wa Mbeya City F, Kinnah Phiri amethibitisha kuwa mlinda mlango mahiri wa kikosi chake Juma Kaseja hatakuwa sehemu ya nyota watakaoiwakililisha City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba Sports alub uliopangwa kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

JUM

Kocha Phiri aliongea na mtandao wa Taarifa.co.tz kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda mjini Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa karibu na familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.

“Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku kadhaa za kubaki nyumbani kushughuliki,” alisema Phiri.

Source: taarifa.co

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents