Burudani

Juliana Kanyomozi: Mwanamke hana jeuri ya kumkatalia mpenzi wake kupiga picha za faragha (utupu)

Muimbaji wa Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana na masuala mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG.

Juliana-for-Satisfashion-UG-4

Miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni pamoja na kuvuja kwa picha za utupu za muimbaji mwenzie wa Uganda, Desire Luzinda. “Kwanza kabisa katika kesi nyingi kamwe huwa sio kosa la mwanamke,” anasema Juliana.

“Kama wewe ni mtu mzima na umempenda mtu unajua kuwa hakuna kikomo cha kipi kitatokea kwenye chumba binafsi cha watu wazima wawili. Kama hautaenda mbali zaidi kumfurahisha mwanaume wako, atakuacha na kisha utahukumiwa kwa hilo,” aliongeza.

“Pindi mwanaume anapovunja uaminifu na kuamua kushare vitu hivyo siri kwa dunia nzima na kutumia vyote dhidi ya mwanamke – ndio maana bado tuna safari ndefu kama wanawake kukemea tabia hiyo.”

“Nachukizwa na wanaume wa aina hii. Wanatia aibu. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa ni wanawake pekee ndio wanaokuwa wahanga kwenye visasi hivi vya mashambulizi ya porn. Unapofanya kitu kama hicho kwa mwanamke, hauwaumizi wanawake wote tu bali pia mama yako, mabinti zako na dada zako.”

Juliana alitolea pia mfano wa udukuzi uliofanyika nchini Marekani na kudai kuwa pamoja na picha za wasanii mbalimbali kuvuja hakuna chombo cha habari cha kuaminika kilichozianika.

“Inanisikitisha hapa nyumbani, kinyume chake ndio kinatokea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents