Habari

Jukwaa la Wahariri laihoji serikali kuhusu kufungiwa kwa Radio 5 na Magic FM

JUKWAAA+PICHA
1.3 Katika tukio la kufutwa kwa mawio, tulihoji ukubwa wa kosa la gazeti hilo kiasi cha kufutwa. Leo hii tunahoji tena ukubwa wa makosa na pengine historia ya radio husika siku zilizopita. Ndiyo maana tunasema hili la sasa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru wa habari.
1.4 TEF inachukulia hatua hii kama mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru vyombo vya habari nchini na tunashindwa kuelewa dhamira ya serikali ya awamu ya tano kwa sekta ya habari nchini. Kinachoonekana ni kutumia kila aina ya sheria iliyopo kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Kimsingi TEF hatuoni nia (spirit) wa malezi katika uamuzi wa waziri huyo.
2.1 Utaratibu uliotumiwa na Waziri kufikia uamuzi huo, umekuwa wa makosa yaleyale ya siku zote. Pamoja na kwamba vyombo vya habari hufanya makosa, lakini hata pale makosa yanapotokea taratibu za kuyashughulikia lazima zizingatie misingi ya utawala bora, haki na demokrasia.
2.2 Mfumo wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaaluma katika vyombo vya habari ni kandamizi kwani unamfanya Waziri kuwa na mamlaka ya kutoa adhabu kwa kuzingatia mtizamo wake, hata kama mtizamo huo unakinzana na misingi ya taaluma.
2.3 Kimsingi uamuzi wa Mh. Nnauye unaonekana hauna nia njema ndani yake kwani Kifungu cha 28 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) alichotumia kutoa adhabu hiyo, hakimlazimishi kufungia Vituo vya Radio kama alivyofanya.
2.4 Kosa la vituo hivyo kwa mujibu wa Waziri ni Uchochezi, lakini hakuweka bayana maudhui ya vipindi au habari ambazo zilivifanya vituo hivyo ‘kutiwa hatiani’ na baadaye kufungwa kwake kwa muda usiojulikana. Kwa sababu hiyo si rahisi kwa waandishi wengine wa habari kujifunza kwa makosa ya wenzao kwa kuwa mchakato uliotumika kushughulikia suala hilo umebaki kuwa siri ya waziri.
2.5 Tunapinga uamuzi wa serikali kuvifungia vituo hivyo sababu na tunatoa mwito kwa Waziri Nape kutafakari upya suala hili na kuachana kabisa na dhamira hiyo isiyokuwa na tija kwa nchi yetu.
NEVILLE MEENA
KATIBU WA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents