Burudani

Jua Cali apanga kumshirikisha Joh Makini

Rapper kutoka nchini Kenya, Jua Cali amesema anatamani kumshirikisha Joh Makini kwenye album yake mpya iitwayo Mali ya Umma inayotarajiwa kutoka October waka huu.

jua-kali

Akizungumza na 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Jua Cali alisema akimpata Joh Makini na akashirikiana naye atafurahi.

“Album itatoka October, September,” alisema. “Jina la album inaitwa Mali ya Umma (Public Properties). Najaribu kumtafuta Joh Makini, huyo ndio nataka kufanya naye kazi yuko sawa kabisa, so nikimpata nitashukuru sana,” alisisitiza rapper huyo.

Jua Cali alifahamika zaidi nchini kwa nyimbo kama Kwaheri, Bidii Yangu na zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents