Burudani

Joto la Dar lamsababisha Fid Q apunguze rasta zake, apanga kuzikata kabisa

Rapper Fid Q ameamua kupunguza dreads zake na kudai kuwa atakaponyooa kipara watu wasimshangae.

10731746_1495626354048255_2043735250_n

Fid Q ameimbaia XXL ya Clouds FM kuwa joto la Dar linamtesa akiwa na rasta ndefu.

“Ni suala la ki-hali ya hewa zaidi,” amesema Ngosha. “Unajua zile dread zilikuwa ndefu kidogo na zinafunika shingo kwahiyo nikaona sio mbaya kama nikizipunguza na kunisaidia kuwa muonekanao mpya. Yote na yote huu ni mwanzo tu ninaelekea kwenda kwenye ‘dongo’ kabisa kwa sababu nimetokea kupenda kwa jinsi kichwa kinavyopigwa upepo mzuri. Ni mimi mwenyewe nimeamka nikasema ‘dah! najitesa zaidi’ sana sana maeneo ya shingoni ninapokuwa natokwa na jasho, ndo nikazikata. Huu mwanzo tu naelekea kwenye dongo,” ameongeza.

“Kwahiyo mtaanza kwa kuona hivi baadaye nitaanza kuvaa kofia kwa wingi halafu litakuja dongo halafu nitavaa kofia ili watu wasishtuke.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents