Burudani

Joti Mbioni Kufungua Studio

joti_mic

 

Msanii wa Sanaa ya maigizo na burudani za vichekesho ambaye anafahamika zaidi kama joti inasemekana yuko mbioni kufungua studio ya kurekodia muziki.

Kwa mujibu wa habari za chini ya kapeti ambazo bongo5 imezikamata mchekeshaji huyo ambaye anaunda kundi la vichekesho la komedi anatarajiwa kufungua studio hiyo maeneo ya Biafra wilaya ya kinondoni jijini Dar-es-Salaam.

Studio hiyo ambayo inasemekana iko katika hatua za mwisho mwisho za matengenezo inatarajiwa kuwa moja ya sehemu zake za kujipatia kipato cha ziada imesha anza kutangazwa chini chini pamoja na kutambulishwa kwa baadhi ya wasanii wa miziki ya kizazi kipya.

Kwa sasa bado haijafahamika ni mtayarishaji gani wa muziki ambaye ndio atakuwa akifanya shughuli za utengenezaji wa muziki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents