Burudani

Joslin afunguka kuhusu mipango ya kuachia albamu pamoja na kundi la Wakali Kwanza

Baada ya kurudi kwenye muziki na wimbo wa ‘Only You’ kufuatia ukimya mrefu, Joslin amefunguka kuhusu mipango yake ya kuachia albamu pamoja na mipango ya kundi lao la Wakali Kwanza.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa yupo kwenye mipango ya kuachia albamu yake mwaka huu pamoja na ile ya kundi huku akimtaja Q Jay ambaye aliwahi kudaiwa kuachana na muziki wa Bongo Fleva kurudi katika kundi hilo wakiungana pamoja na Makamua.

“Nyimbo kama nane ninazo, Wakali Kwanza nyimbo kama 10 tayari tumeshafanya na bado tunaendelea kurekodi kwa kuwa lengo na nia ni kuachia albamu. Mwaka huu huu Mungu akipenda nitaachia albamu yangu na ikiwezekana na ile ya kundi pia,”amesema Joslin.

Joslin ameongeza kuwa mbali na ahadi yake aliyowahi kuahidi ya kuzifanyia video nyimbo zake za zamani ambazo hazikuwa na video amepanga kufanya remix ya nyimbo zake kubwa tatu ikiwemo ‘Niite Basi’, ‘Perfume’ na ‘Mshikaji Mmoja Hivi’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents