Michezo

Jose Mourinho adai Chelsea itachukua ubingwa wa EPL

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema klabu ya Chelsea inaweza kuangazia michuano ya FA kwani tayari wanajua ni mabingwa wa Ligi ya Premia.

Vijana hao wa Antonio Conte, ambao watawakaribisha United Stamford Bridge katika robo fainali Kombe la FA mwezi Machi, wamo mbele kwa alama nane katika msimamo wa ligi na bado wamesalia na michezo 13.

Chelsea waliendelea na makali yao kwa kuchapa Wolves 2-0 katika raundi ya tano Kombe la FA, huku United wakitoka nyuma na kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Blackburn.

“Kombe la FA ni kitu muhimu kwao,” amesema meneja wa zamani wa Blues, Mourinho.

Chelsea wanapigiwa upatu kushinda ligi kwa mara ya pili kwa miaka mitatu baada ya Mourihno kutwaa ubingwa akiwa nao msimu wa 2014-2015.

“Chelsea wanaweza kuangazia vyema michuano ya FA, kwa fikira zangu kwani ni mabigwa na hawana michuano mingine inayowatatiza. Kombe la FA ni muhimu kwao.

Katika msimu wa kwanza kwa meneja Mourinho uwanjani Old Trafford, ameongoza klabu hiyo kuwa miongoni mwa timu 32 bora katika ligi ya Europa, ambapo kwa sasa wamo kifua mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya Saint- Etienne ya Ufaransa .
United wanashikilia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Premia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents