Burudani

Jose Chameleone kufanya show Uganda ya shilingi 1000, kuwafidia watakaoshindwa kumudu show yake ya December ya milioni 1

Mwanamuziki mkubwa wa Afrika, Jose Chameleone anatarajia kufanya show kubwa mwezi Desemba kwaajili ya mashabiki wa ‘kishua’ jijini Kampala, Uganda iliyopewa jina la ‘1Man 1Show 1Million’ ambayo kiingilio chake kitakuwa shilingi milioni 1 za Uganda (Tsh 630,000/=) kwa mtu mmoja.

chm

Lakini baada ya mashabiki wake walio wengi wa hali ya kawaida kulalamika kuwa kiingilio hicho ni kikubwa sana kwao na wangependa kuhudhuria onesho hilo, Chameleone ameamua kuwaandalia show yao maalum ambayo itakuwa ya kiingilio cha chini kupita kawaida, shilingi 1,000 ya UG kwa mtu mmoja sawa na Tsh 630/= ambayo nayo ameipa jina la ‘1 Man 1 Show 1 Thousand’.

“Started as a Rumour, I CONFIRM now!!! The sky has never been no limit!!! For my folks that will miss out on this SHOWDOWN, Never worry there is another charity do coming up soon!! 1 man ,1 show,1 thousand. Those up for this, We are Loading Ugandan music on Record,” aliandika kwenye ukurasa wake wa facbook.

Baada ya kuthibitisha juu ya show hiyo ya buku 1, mashabiki wengine walianza tena kuponda wakidai kuwa kiingilio hicho ni kidogo sana hivyo itajaza sana watu na kugeuka kuwa kero, Kwa mujibu wa Uganda Online.

Hata hivyo haijafahamika show hiyo ya charity itafanyika lini. Show ya 1Show 1Man 1Million inatarajiwa kufanyika Desemba 18.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents