Burudani

Jokate: Hasheem was my first real love, Nilikuwa naogopa sana kumpoteza

Muigizaji wa filamu, VJ wa Channel O Tanzania, mbunifu wa mavazi na mjasiriamali, Jokate Mwegelo aka Kidoti amekiri kuwa mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet ndiye mwanaume aliyewahi kumpenda zaidi maishani mwake.

Jokate_by_jarry85

Jokate ambaye ni cover girl kwenye jarida jipya la Vibetz, alifunguka kuwa japo uhusiano wake na Hasheem ulidumu kwa miaka mitatu, walifanikiwa kuufanya usijulikane sana kwa wengi na walikuwa wakipendana sana.

“With Hasheem, I think it was more than love. He was my first real love,” aliliambia jarida hilo.

“Siku zote nilidhani he was my soulmate. Kiukweli nilimpenda sana. He is like the only guy I would drop anything at anytime for. Nilikuwa tayari kufanya lolote kwaajili yake, that’s how deep I loved that guy,” aliongeza.

“Nilimpenda kiukweli Hasheem, and yes kama mwanamke mwenye kutaka kufanikiwa I’m drawn to ambitious/successful men, you know the go getters but my family haikunilea katika maadili ya kujenga mahusiano yoyote katika mhimili wa fedha,” Jokate alieleza kujibu swali kama aliamua kuwa na Hasheem kwasababu ya fedha zake. “I had never wanted to use Hasheem, all I wanted was to love him.”

Hata hivyo, Jokate anadai kuishi mbali na Hasheem anayechezea timu ya Oklahoma City Thunders, ni moja ya sababu iliyochangia kuvunjika kwa uhusiano wao.

“Yes kuishi mbalimbali pia inaweza kuwa sababu japo ndogo iliyochangia kuvunjika mahusiano yetu cause sometimes I would hear a lot of stuff and that would upset me. Nilikuwa naogopa sana kumpoteza, I ended up doing vitu vya kijinga kama dating Diamond. I had issues with Hasheem na Diamond came in picture. It was a very frustrating time for me. I was super confused. I cried for a whole year. Like every night I would just cry like crazy.”

Jokate alikanusha pia kuwa kwa kuanzisha uhusiano na Diamond hakunuia kumuumiza Wema Sepetu ambaye kipindi hicho walikuwa wapenzi.

“I never intended to hurt anyone, lakini hata hivyo Diamond gave me the impression kwamba Wema alikuwa anamcheat and he wanted to leave her. Sikudhamiria kumuumiza Wema, huo ndio ukweli,” Jokate ameliambia Vibetz.

Kwenye jarida la Mzuka lililopita, Wema alisimulia jinsi alivyogundua uhusiano wa Jokate na Diamond.

“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate .Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.

Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu,” alisema Wema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents