Burudani

Jokate atoa ukweli juu ya tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na producer Lucci

Mrembo na mwanamitindo Jokate Mwegelo anayejulikana pia kama Kidoti ameamua kuvunja ukimya kwa kutoa maelezo juu ya tetesi zilizoenea mitaani kuwa kuna uwezekano mrembo huyo kuwa (au wamewahi kuwa ) na uhusiano wa kimapenzi na producer Luciano Gadie Tsere aka Lucci.

lucci n jokate

Haya yote ni matokeo ya video ya wimbo wa wawili hao ‘KAKA DADA’ iliyotoka hivi karibuni na kuonekana kuwashtua baadhi ya watu kutokana na jinsi walivyoonekana kuwa na ukaribu wa ‘zaidi’ ya kuigiza kwenye video,na kufanya watu wahisi Jokate na Lucci ni wapenzi.

Kupitia Instagram Jokate ameandika:

“Okay leo nimeamua kupitia page yangu ya Instagram ku-address the following pressing matters kwenye ulimwengu wa majungu. 1. Luciano Gadie Tsere is NOT my LOVER and noooo hatumegani kisela. Na hata kama it were true inakuhusu nini. Sioni ishu. Kwenye Sanaa kuna kitu kinaitwa kuweka uhalisia. And that’s what we did na KAKA DADA. I respect Lucci. Ni kaka yangu na tunafanya kazi nyingi sana zinakuja. Kuna watu wanefungua mpaka BBM group to discuss me and Lucci and this so called affair. Jamani kuliko maneno tufanyeni Kazi kuendeleza nchi yetu 2. Sijifanyi mtakatifu. Ila najitahidi kufanya matendo yanayompendeza Mungu. Na kwasababu kama binadamu sina ukamilifu basi only God can really judge me cause ndio anajua moyo wangu kuliko binadamu yoyote yule. Ila I’m a pretty good girl to be honest. Najaribu. Kwa nyinyi walimwengu don’t be fooled by my PRETTY BABY FACE I know what I want, am fierce and I don’t take trying to tarnish my image easily. So kindly don’t mess with KIDOTI. Msione mtu mkimya mkajua ndio wa kumuonea. Still waters run deep 3. Yes there’s some guy I’m checking out. Like any other female I deserve love cause I got so much love to give hey. So whoever it is tafadhali tusiharibiane kwa maneno maneno. Have a blessed evening!!!..”

jokate insta

Hivi karibuni, naye Lucci alilizungumzia suala hilo.

Kama hujabahatika kuiona video ya ‘Kaka Dada’ iliyofanyika nchini Kenya na kampuni ya Ogopa itazame hapo chini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents