Burudani

Jokate aongelea mipango ya kuzindua tena nywele zake, kutoa movie zake 2 mwakani na kuhusu video ya Kaka Dada

Jokate Mwegeko aka Kidoti amesema anatarajia kuzindua tena nywele zake za brand ya Kidoti. Akiongea na Salma Msangi jana jioni kwenye kipindi cha Afrika Kabisa cha Magic FM, Jokate alisema baada ya kupata ‘mrejesho’ (feedback) kuhusiana na nywele zake za mwanzo, anajipanga kutoa nywele bora zaidi.

kidoti

“Kuna vitu ambavyo nimevirekebisha kwahiyo nakaribia tena kurelaunch hivi karibuni,” alisema. Pia alisema anakaribia kufanya filamu zake yeye mwenyewe.

“Kama mbili hivi nitafanya kama sio mwisho wa mwezi huu, mwanzoni mwa January.”

Katika hatua nyingine Jokate alisema pamoja na kwamba video ya wimbo wake na Lucci ‘Kaka Dada’ ilikoselewa, hakuna kilichompa shida.

Day4

“Ukifanya sanaa lazima ufanye ile inayogusa watu na ukitaka kugusa watu ni lazima ufanye kitu ambacho kinaendana na uhalisia ndio kile tulichoenda kukifanya. Lakini yale mengine yote ni matokeo tu. Watu wanaweza wakaigiza muziki love scenes halafu ni mbaya hazina chemistry, hauitendei haki sanaa. Mi nafurahia sababu naamini tumeitendea haki sanaa. Sidhani kama kuna video ambayo imeitendea haki sanaa kama hiyo ya kwetu,” alifunguka mrembo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents