Burudani

Jokate achukua nafasi ya Vanessa Mdee kwenye ‘The One Show’ ya TV1, atashirikiana na Ezden Jumanne

Jokate Mwegelo amechukua nafasi ya Vanessa Mdee kama mtangazaji wa show mpya ya kituo cha TV1 kilichozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Awali Vanessa ndiye aliyekuwa amechukuliwa kuendesha kipindi hicho na tayari alikuwa ameanza kurekodi vipindi. Haijulikani mabadiliko hayo yamesababishwa na nini.

Vanessa

Jokate Mwegelo atakuwa akiendesha kipindi hicho akishirikiana na mtangazaji wa zamani wa Kiss FM na Times FM, Ezden Jumanne aka The Rocker.

MMG28728
Ezden Jumanne akiongea na waandishi wa habari leo kwenye uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika jijini Dar. Pembeni yake ni Jokate Mwegelo

MMG28706
Jokate Mwegelo akiongea na waandishi wa habari

Show hiyo ni version ya Tanzania ya show kama hiyo inayorushwa kwenye kituo cha TV cha Viasat cha Ghana ambacho nacho kinamilikiwa na kampuni moja inayoimiliki TV1, MTG ya nchini Sweden.

Picha: Othman Michuzi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents