Burudani

John Legend atangaza ziara yake ya ‘Darkness and Light’

Msanii wa RnB wa Marekani, John Legend ametangaza kuanza kwa ziara yake ya Darkness and Light ambayo atazunguka katika miji ya Marekani.

Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka katika miji ya Atlanta, Phoenix, Los Angeles, Minneapolis, New York na Boston na inatarajiwa kuanzia katika mji wa Miami, Mei 12 mwaka huu na kumalizikia katika mji wa Los Angeles, Juni 30.

Darkness and Light ni jina la albamu ya tano ya muimbaji huyo ambayo ameiachia Disemba 2, mwaka jana na ilifanikiwa kushika namba 14 kwenye chati za Billboard 200.

Wakati huo huo John Legend anatarajiwa kutumbuiza kwenye tuzo za 59 za Grammy ambazo zitafanyika Jumapili ya Februari 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents