Burudani

Joh Makini na G-Nako wafanya kolabo na Sauti Sol

Baada ya kufanya wimbo na msanii wa Nigeria, Chidinma, Joh Makini ameongeza wigo wa kolabo zake za kimataifa na usiku wa kuamkia Jumamosi hii, akiwa na Mweusi mwenzie, G-Nako, wamerekodi wimbo na kundi la Sauti Sol la nchini Kenya.
10561184_156093537899165_291287605_n

“Studioni mpaka alfajiri ya leo na @Sautisol @fancy_fingers @savaramudigi @chimano @bienaimealusa @fundifrank #hakunakulala #Mwenyezi Mungu ni muaminifu #kituimepikwa,” ameandika Joh Makini kwenye picha aliyoweka Instagram akiwa na members wanne wa kundi hilo.

Naye mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, Savara Mudigi Delvin amepost picha hiyo na kuandika: Another night full of productivity. We made a tune. Big collabo with @Joh_makini and @Gnakowarawara @sautisol @fundifrank @chimano @bienaimealusa @fancy_fingers #greatness #seeyourlife #SolDanceMusic.”

Joh Makini yupo jijini Nairobi alikoenda kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa.

1941202_1443889615875384_1402994678_n
Joh Makini, G-Nako, Chidinma na producer RKay wa Kenya wakiwa studio baada ya kurekodi wimbo. “Shukurani sana kwa producer @rkaykamanzi @gnakowarawara na mwanadada @chidinmaekile leo nimemuimbisha kiswahili asante @cokestudioafrica kwa kutuleta pamoja #cokestudioafrica,” aliandika Joh Makini kwenye picha hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents