Burudani

Joh Makini awashauri waongozaji wa video wa Bongo kujituma zaidi

Hitmaker wa Don’t Bother, Joh Makini amewataka waongozaji wa video wa ndani kujitahidi ili waende sambamba na waongozaji wa nje wanaofanya vizuri kwa sasa.

joh makini

Joh Makini amekiambia kipindi cha Planet Bongo kinachoruka kupitia EATV kuwa, Tanzania imefika sehemu nzuri lakini waongozaji wanatakiwa kuongeza zaidi juhudi.

“Ni lazima tuhakikishe tunafika kwenye level ambayo tutakubalika dunia nzima,” alisema Joh.

“Mimi naamini tunaweza na tayari wameshaonesha njia kwa kufanya vizuri. Kikubwa ni kutoridhika kwenye level waliopo kwa sababu inabidi watu wakaze ili tuweze kwenda sambamba na watayarishaji wa nje ambao wanafanya video kubwa. Kwa sababu sio ukienda South Africa directors wote wanafanya vizuri, ukiangalia directors ambao wapo kwenye soko wanahesabika. So inabidi watu wafanye kazi kwa kujifunza na kujituma sana kila siku,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents