Burudani

Joh Makini awatahadharisha mashabiki wake juu ya akaunti feki ya Facebook

Rapper Joh Makini amewatahadharisha mashabiki wake kutowaamini watu wanaotumia jina lake kuuza biashara zao mitandaoni.

Joh

Kupitia mtandao wa Facebook imefunguliwa akaunti ambayo inatumia jina la msanii huyo huku ikitangaza matangazo ya kuuza biashara ikiwemo viatu ambayo hata hivyo hitmaker huyo wa Don’t Bother amedai kuwa haitambui.

french-montana-remy-ma-fat-joe

Kupitia akaunti yake ya mtandao huo, Joh Makini ameandika:

TAHADHARI!! AKAUNTI HII SIO YANGU NI MATAPELI NAENDELEA KUSISITIZA SINA BIASHARA YOYOTE NINAYOIFANYA KUPITIA FACEBOOK PAGE YANGU..
JIHADHARI NA WEZI HAWA WA MTANDAONI..

Wezi wa mtandaoni wameonekana kutembea karibu na rapper huyo ikiwa ni siku chache zimepita tangu walipoweza kuidukua akaunti yake ya Instagram mara mbili kwa kipindi cha miezi miwili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents