Burudani

Joh Makini asema 2014 umekuwa mwaka wa mafanikio kwa muziki na maisha ya wasanii

Mweusi Joh Makini amedai kuwa juhudi za wasanii katika muziki zimeufanya mwaka 2014 kuwa wenye mafanikio kwao na nchi kwa ujumla.

10691617_299232690273582_385333800_n

Joh amekiambia kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio kuwa mwaka huu ni mwaka yalipofanyika mapinduzi makubwa katika muziki.

“Industry imekuwa kubwa, sasa hivi ni biashara nafikiri ndo umechangia sana wasanii kufanya vizuri na kufanya kazi katika ubora na kusababisha mwaka huu kusema muziki wetu umeenda mbali tofautisha na miaka mingine,” amesema. “Mimi katika miaka ambayo naweza kusema imekuwa na mafanikio kwa wasanii na hata kwa tasnia nzima ya muziki moja katika kitu kikubwa kilichochangia ni biashara ili iwe kwenye soko lazima ufanye kazi nzuri. Kwahiyo wasanii wamejituma sana kufanya kazi nzuri na kufanya video nzuri. Umeona wasanii wanafanya kolabo na international artists yote hiyo ni katika kutafuta ubora ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko kwahiyo nafikiri biashara imeboost pia. Mimi binafsi nawapongeza wasanii kwa kazi kubwa ambayo wameifanya mwaka huu.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents