Burudani

Joh Makini aizungumzia video ya ‘I See Me’ baada ya ubora wake kukosolewa

Joh Makini ameamua kuyajibu malalamiko ya baadhi ya mashabiki wake wanaodai kuwa video ya ‘I See Me’ imekuwa chini ya kiwango.

Nikki wa 2,Joh Makini na G.Nako wakiwa katika project yao mpya ya muziki

Joh Makini ameiambia Enewz ya EATV kuwa ukubwa wa wimbo huo ulisababisha mashabiki kuwa na video yao kichwwani.

“Kinacho wakosti watu wengi ni kwa sababu kila mtu amekuwa akitengeneza picha yake kichwani ya video ya wimbo,” alisema. “Sasa inakuwa tofauti kutengeneza picha kwa kila mtu. Kuna watu wengi wametoa maoni yao na wamekubali video na wameipenda na sisi tumekubali ile concept ya design ile ni concept ya mazingira, yaani najua kitu ambacho watu walitaka kukiona kwahiyo tumeamua kwenda tofauti. Wakati mwingine kwenye muziki unatakiwa kuwa tofauti na usiogope challenge na kufanya kitu tofauti. Suala la low budget video tumeshoot Nairobi na imelipwa hela ambayo siwezi kukwambia kwa sababu hatupendagi hivyo vitu lakini labda ukimpigia director Enos Olik.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents