Jinsi mashabiki wanavyomsulubu TID kwa kujiondoa kwenye show ya Jaydee

Katika maisha kuna wakati watu huchukua maamuzi magumu kwa kile wanachoamini yanaweza kuwaepusha na shida kubwa za baadaye. Maamuzi hayo magumu yanaweza kubadilisha mustakabali na kuufanya kuwa mzuri ama pia kuufanya kuwa mbaya kulivyo walivyotarajia.

Top indar

Kabla hatujangia kwenye kile tunachokwenda kukisema, tungependa kusema kuwa muziki wa Tanzania sasa hivi umefika katika wakati mgumu kidogo hasa kwa vyombo vya habari kuwasilisha habari kuhusiana pande mbili zilizopo kwenye mgogoro huu unaoendelea.

Hii ni kwasababu imetulazimu kujitahidi kuandika habari kwa usawa ili kuepusha kuonekana kuegemea upande mmoja. Kwa muda mrefu Bongo5 imejitahidi sana kuzipa pande zote mbili fursa ya kuandikiwa ‘upande wao wa story’ (their side of the story) ili kuwapasha wasomaji wetu kipi kinachooendelea ambao wenyewe ndio wenye haki ya kuchagua upande wa kuegemea.

Jana Khalid Mohamed aka Top in Dar alichukua uamuzi mgumu wa kujiondoa kwenye list ya wasanii watakaoisindikiza show ya miaka 13 ya Lady Jaydee. TID alitoa sababu tatu. Ya kwanza ikiwa ni kuwa na mkataba mwingine unaolipa kuliko aliopewa na Jaydee, ya pili ni kutotaka kuwa katikati ya ugomvi usiomhusu na ya tatu ni kutokana na kuwa na mipango ya kuoa. Sababu hiyo ya tatu kwa wengi imepokelewa kwa mshangao mkubwa kwamba inahusiana vipi na show ya Jaydee?

“Dude u so wack, kipindi unaanza muziki nilikua nakuelewa bt nt anymor..u xo unprofessional,” ameandika shabiki mmoja kuelezea alivyouchukulia uamuzi wa TID.

“Eti u got beta payin contract, wtf contract gani hizo u talkin bout, its nat always bout the money, sometimes it aint fo the money but support.. Eti u dnt wana b a cnflict in between n yako yanakushnda, seriously yanakushnda u nid help bgtymz. Eti una mpango wa kuoa, nigger is the wedding on the same day as jd show?!n ulipokua unakubal haukujua that u gon get married? Criously that TOP IN DAR SHOULD CHANGE TO FLOP IN DAR.. Nigger u way outa yo own.”

“Those are lame excuse to come from you TID,” ameandika mwingine aitwaye Abdul Karim Adam. “Excuse yourself for a better reason NOT getting rid of your friends. It means that quids (Money) comes first before you friends and that you don’t want to be involved in the purportedly conflicts between the two, It means that you already know the truth and afraid to be associated with JIDE (cowardice of the highest order). and lastly getting married. Why now?!! when you needed most you bring the marriage thing. Remember a friend in need is a friend in deed. you have your way of getting things but you should always know that no man is an island. Leo ni JIDE Kesho……………….. Tafakari.”

Katika habari tuliyoandika jana kuhusu uamuzi huu wa TID, zaidi ya watu 80 wamecomment na asilimia 99 ya wachangiaji hao wamekuwa disappointed na uamuzi huo wa TID. Pia mpaka sasa comments kwenye ukurasa wa Facebook wa TID kuhusiana na uamuzi wake zimefikia zaidi ya 420 ambapo asilimia 99 zinamponda. Kwa namna yoyote uamuzi huu utamcost TID. Amepoteza mashabiki wengi watakaonza kumuona kama ‘kigeugeu’. Lakini mwisho wa siku kila mtu ana maisha yake na yupo huru kuamua anachotaka ilimradi kwake anaamini ni uamuzi sahihi. Mashabiki waheshimu uamuzi wa TID.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents