Bongo Movie

Jini Kabula na Jack Pentzel wakanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja


Kwa muda mrefu waigizaji wa kike wa Bongo Movies, Jack Pentzel na Miriam Jolwa aka Jini Kabula wamekuwa wakisakamwa na skendo ya usagaji kutokana na picha iliyosambaa kwenye mtandao inayowaonesha wakibusiana.

Hata hivyo wote wameendelea kukanusha kutojihusisha na vitendo hivyo kwa kudai kuwa walikuwa kazini.

Akiongena na kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, Jack amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Miriam kwakuwa zile ni picha zilizochukuliwa wakati wakishoot movie.

“Mi mwenyewe nimezisikia kama wewe ulivyozisikia, lakini ukweli ni kwamba mimi ni msanii, ni msanii wa filamu nafanya kazi za kuelimisha jamii, kwamba jamii ntaifundisha kwamba ifanye hivi ntaikosoa ifanye hivi. Kwahiyo zile ni picha ambazo zilipigwa wakati tupo location, na sio kwamba zile picha walizoziona wao ndio kile kitu sisi tulichokuwa tunakifanya. Sisi tulikuwa tunaigiza, hakuna uhalisia wowote wa kitu tulichokuwa tunakifanya”, alisema.

“Mimi nina mtu wangu, mimi nina mpenzi wangu, kwanza siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzangu, kwasababu atanifanya nini mpaka mimi niridhike?”

Kwa upande wake Miriam, naye alikanusha kuwa na uhusiano na mwanamke mwenzake na kusisitiza kile alichokisema mwenzie.

“Ni kweli hizo picha zipo, lakini sio kama namaanisha mimi na Jack Pentzel tulikuwa tunafanya huo uchafu. Hiyo ni movie tulikuwa tunacheza, mimi nilikuwa kama namuapproach Jack, yaani mimi ndio yule mwanamke msagaji halafu yeye ndio demu wangu. Na hiyo movie sijui kwanini inachelewa kutoka,” alisisitiza Miriam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents