Habari

Jini Kabula, Isabella na Rashida Wanjara waanzisha kundi la muziki

Ladies and gentlemen, boys and girls let’s give Scorpion Galz a round of applause as they hit the stage! Siku si nyingi washereheshaji wa concerts watasikika wakisema hivyo kwa kundi jipya la madiva walioamua kujaribu bahati zao kwenye muziki.

Scorpion Galz litaundwa na Jini Kabula, Rashida Wanjara na Isabella ambao wote waliwahi kushiriki katika mashindano ya umiss.

Kwa mujibu wa akinadada hao, wameamua kufanya muziki si kwaajili ya kuuza sura bali ni kusaka mshiko kwakuwa muziki unalipa.

Inadaiwa kuwa video ya wimbo wao utakaowatambulisha nchini itatoka hivi karibuni ambapo mavazi yao yanasimamiwa na kampuni ya Kidoti Fashions ya Jokate Mwegelo.

Rashida Wanjara aliwahi kuwa Miss Mara ambaye pia aliingia ‘top 5’ ya Miss Tanzania 2000/01.

Jini Kabula ambaye jina lake halisi ni Mariam Jolwa anafahamika zaidi kwa uhusika wake kwenye tamthilia ya Jumba la Dhahabu.

Will they make a hit?Isabella akiwa na mbunifu wao wa mavazi, Jokate Mwegelo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents