Habari

Jeshi la Polisi lawaonya wananchi wanaofanya manunuzi kwa njia ya mitandao

Jeshi la polisi nchini limewataadharisha wafanyabiashara na wananchi wanaofanya manunuzi au kuuza bidhaa kwa njia za mtandao kuwa makini na matapeli wanaotumia mitandao kufanya uhalifu vikiwemo vitendo vya wizi.


Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba na kutoa tahadhari hiyo kutokana na kuwepo kwa matukio mengi ya watu kuibiwa fedha zao wakati wa kuuza au kununua bidhaa kwa kutumia mitandao.

“Watu wamekuwa wakifanya biashara kwa njia za mtandao na matokeo yake wanajikuta wanaingia kwenye kutapeliwa kwenye kuibiwa kwasababu tu ametuma pesa kwa mtu ambaye hamfahamu, amefanya biashara na mtu ambaye hamfahamu yani wamewasiliana tu kupitia mtandao,” alisema Bulimba.

“Kwamba mimi nafanya biashara mbili tatu, mimi nauza kitu fulani nitumie pesa kiasi fulani ntakutumia mzigo, tunaomba wananchi wawe makini na hili suala kwasababu tumepokea matokeo mengi ya wananchi kutapeliwa kwa njia ya mtandao”.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents