Habari

Jeshi la Polisi lapiga marufuku wananchi kukusanyika kwenye vituo vya polisi

Jeshi la Polisi limepiga marufuku tabia ya wananchi kukusanyika katika vituo vya polisi pindi baadhi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wanapotakiwa kufika kwenye vituo vya polisi kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Polisi ACP Advera Bulimba ambaye amesisitiza kuwa mtu au kikundi chochote cha watu watakaokusanyika katika kituo cha polisi bila kuwa na sababu ya msingi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi nchini tunakemea vikali baadhi ya watu, baadhi ya wananchi wanaposikia baadhi ya watuhumiwa wanaitwa kwenye vituo vya Polisi kwenda kukusanyika kwenye vituo vya polisi, kwa lengo la aidha kuwaangalia watu hao au kufanya ushabiki au mbwembwe za aina yeyote jambo hilo hatuta liruhusu na tumetoa maelekezo mikoa yote kuhakikisha kwamba yeyote atakae fanya hivyo ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria,” alisema ACP Bulimba.

Rais Dkt John Magufuli pia alipiga marufuku wananchi kukusanyika vituo vya Polisi wakati akiongea kwenye hafla ya kuwaapisha maafisa mbalimbali Jumapili jijini Dar es Salaam.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents